Mifumo kandamizi kwenye sekta ya kilimo ikemewe (GF17/TJ17)

LUCIA  Akaro,  mwakilishi  wa  EKAMA  Development  Foundation Tanzania  amesema kuna  haja ya  mifumo kandamizi  kwa  wanawake  kukemewa .

Akaro ametoa kauli hiyo wakati akiwasilisha mada ya ardhi,kilimo, uzinduaji,uchimbaji madini na mabadiliko  ya  tabia  nchini  kwa wanawake  na makundi yaliyoko pembezoni  wakati  wa  warsha  zinazoendelea  katika tamasha la jinsia la 14  liloloandaliwa na mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP – Mtandao )

“Kundi la wanawake ndilo kundi linaloathirika zaidi na mabadiliko ya Tabia nchi  Katika  kupambana na  ukatili  wa  kijinsia.  Kuna haja  ya  kuanzisha  majukwaa mbali  mbali ya  utoaji  wa  elimu  kwa  jamii ili kuondokana na unyanyasaji  wa  familia kupitia  ardhi ama mavuno “


Dada Akaro akiendesha warsha katika viwanja vya TGNP Mtandao kwenye TAMASHA LA JINSIA 2017.

Alizitaja  athari zitokanazo na ukatili wa jinsia kuwa ni kupungua kwa nguvu kazi pamoja na kipato cha wanawake kinachopelekea kuwepo kwa umaskini ,kupungua kwa uhifadhi wa chakula na kukosekana kwa muda wa kutosha kufanya kazi shambani kutokana na vitendo vya kikatili .

Katika kutatua changamoto hizo amesema  katika sekta ya kilimo  kuna haja  ya  kuwajumuisha  wanawake  katika mnyororo wa thamani wa kilimo ili kungeza bei ya mazao na kuteneneza nafasi nyingi za ajira . kuongeza jitiada katika kuzuia upotevu wa mazao kipindi cha uvunaji na baada ya uvunaji kwa kuhifadhi  mazao vizuri katika maghala au katika mapipa maalum  na Serikali iongeze bajeti yenye mlengo wa kijinsia  katika sekta ya kilimo.

“Ni muhimu kujumuisha masuala ya mabadiliko ya Tabia nchi katika mipango na bajeti kuanzia ngazi ya serikali za mitaa hadi ngazi ya taifa. Elimu itolewe kwa jamii kuhusu athari za ukatili wa jinsia, Wanaume wahusishwe katika mapambano ya kupinga ukatili wa jinsia,” amesema Akaro.

Aidha, Nembris Mollel mshirikmi wa warsha hiyo amesema   “asasi  zinazoshughulika na harakati za  kumkomboa mwanamke  kuiga mfano  wa TGNP Mtandao  kwa  kuwatembelea  wananchi wa  pembezoni  badala ya  kujikita  mijini pekee.”